Thursday, 8 June 2017

Mwanamke acha kubandika kucha, tumia njia hizi 3 za asili kukuza kucha zako haraka


Kinadada wengi kwa sasa wamekuwa wakipenda urembo miongoni mwa vitu ambavyo wamekuwa wakivipenda pia katika urembo wao ni pamoja na kuwa na kucha ndefu ambapo wengi huamua kubandika kucha bandia.

Kuna baadhi yao hupata madhara au maudhi fulanifulani wanapobandika kucha hizo sasa kutokana na kulitambua hilo leo nimeona nikueleze kuhusu hizi mbinu za kukuza kucha zako kwa njia asili na zitakuwa ndefu na imara tu.

Mambo 3 yakufanya ili kukuza kucha kwa njia asili

1. Jusi ya chungwa
Kamua juisi ya chungwa kwenye bakuli kisha loweka vidole vyako ndani ya juisi hiyo angalau kwa dakika 10, kisha baada ya hapo nawa kwa maji ya uvuguvugu. Fanya zoezi hilo kwa wiki kadhaa hadi utakapoona mafanikio.

2. Juisi ya limao & mafuta ya mzaituni
Andaa juisi ya limao kisha changanya na mafuta ya mzaituni halafu utaloweka mikono yako (kucha zako) kwenye mchanganyiko huo kwa dakika 10. Fanya zoezi hilo hadi utakaporithika na matokeo.

Unaweza pia ingiza kucha zako kwneye kipande cha limao kwa dakika10 kwa wiki kadhaa mfululizo nayo husaidia kukuza kucha na kuzipa uimara zaidi.

3. Mafuta ya nazi
Pata mafuta halisi ya nazi kisha yapashe kwenye moto kiasi yawe na joto la wastani ambao utweza kuweka mikono kwa kuloweka kucha zako kwa dakika 10. Fanya zoezi hilo kwa wiki mbili hadi 3 na utaona jinsi kucha sitakavyokua vizuri na imara.

Kwa maelezo na ufafanuzi zaidi tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment