Friday, 30 June 2017

Namna 4 za kukabiliana na maumivu ya goti


Sehemu ya goti ni muhimu sana kwa mtu yoyote kwani ni moja ya maungio ambayo humsadia mtu kuweza kutembea kwa urahisi, hivyo eneo hilo linapokuwa na tatizo huweza kuwa na madhara kwa mhusika.

Maumivu ya goti huweza kumsababishia mhusika kutembea kwa tabu, kukaa, kukimbi na hata kushindwa kufanya shughuli zake za kila siku ipasavyo.

Leo ninazo hizi njia kadhaa ambazo huweza kumsaidia mtu mwenye maumivu ya goti kupunguza maumivu ya tatizo hilo.

1. Kutumia Kitunguu swaumu

Kiungo hiki kinatambulika zaidi kama kituliza maumivu cha asili, sasa ili kikusaidie kutuliza maumivu ya goti utatakiwa kusaga na kuchanganya na karafuu iliyosagwa na baadaye kuchanganya na mafuta ya alizeti kisha mhusika atatumia mchanganyiko huo kuchua kwenye goti kutwa mara 3 na atapata ahueni.

2. Vitamin B

Mtu mwenye tatizo la maumivu ya goti huhitaji vitamin B kwa wingi ili kupunguza maumivu hayo na vyakula ambavyo ni chanzo cha vitamin hiyo ni pamoja na mayai, samaki, soya pamoja na aina zote za nafaka.

3. Tangawizi

Kiungo hiki kinasifika kwa kutuliza maumivu ya mifupa, hivyo mtu mwenye maumivu ya goti anaweza kuandaliwa juisi ya tangawizi na kunywa asubuhi na jioni kila siku.

4. Mchanganyiko wa mdalasini & asali

Mchanganyiko huu kazi yake kubwa ni kwenda kuchangamsha mzunguko wa damu na hivyo kusaidia kupunguza maumivu ya goti na mifupa kwa ujumla wake.

Mbali na hayo, mambo mengine ambayo huweza kupunguza maumivu yagoti ni pamoja na mazoezi mepesi ya kukunja na kukunjua mguu sambamba na massage kwenye eneo lenye tatizo.

Kamamungependa kujua vipimo vya kuchanganya wakati wa maandalizi wa njia zote kuanzia hiyo ya kitunguu swaumu na karafuu pamoja na mafuta ya alizeti tupigie kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com tutakuelekeza.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment