Tuesday, 6 June 2017

Namna kitunguu swaumu na karafuu vinavyoweza kumaliza chunusi

Moja ya mambo ambayo huwakwaza na kuwakosesha vijana wengi wa kiume na wa kike katika makuzi yao ni pamoja na pale wanapojikuta ngozi zao au mionekano yao inaharibika kwa kusongwa na chunusi.

Kutokana na kulitambua hilo leo nimeona nikueleze hii mbinu  asili ya kumaliza tatizo hilo

Kitunguu Swaumu na Karafuu
Viungo hivi viwili ni viungo vya kawaida kabisa ambavyo wengi wetu naamini tunaweza kuvipata kirahisi katika maisha yetu  ya kila siku.

Namna ya Kuandaa
Saga kitunguu saumu pamoja na karfuu kisha changanya kwa  pamoja kisha tumia mchanganyiko huo kuweka maeneo yenye chunusi huku ukisugua kwa taratibu sana bila kutumia nguvu

Baada ya hapo acha mchanganyiko huo kwenye uso wako kwa dakika 10 kabla ya kunawa na maji safi. Fanya zoezi hilo angalau mara 2 kila siku hadi pale utakapoona mabadiliko au chunusi kuisha kabisa.

Kwa msaada zaidi wa maelekezo unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment