Saturday, 10 June 2017

Nimekuletea faida ya mchanganyiko wa asali, limao na kitunguu majiJuisi ya kitunguu maji ni moja ya  njia mbadala ya kulinda afya ya nywele zako na kuzizuia kukatika, lakini pia kuzifanya kuwa na afya bora.

Lakini unapoandaa juisi hiyo ya kitunguu maji na kuchanganya na asali basi unaweza kupata matokeo mazuri zaidi katika nywele zako.

Jinsi ya Kuandaa
Katakata vitunguu vyako kadhaa, kisha viweke kwenye blenda au mashine ya kusagia halafu changanya na asali kiasi kisha saga kwa pamoja. Pia unaweza kukamulia na limao kidogo ili kukata harufu ya kitunguu ukiweza

Baada ya hapo utapata mchanganyiko mzito ambao sasa huo ndio utautumia kwa kupaka vizuri kwenye nywele zako wakati wa usiku kabla ya kulala.

Hakikisha unapaka vyema mchanganyiko huo na unagusa sehemu zote za kichwa chako, kisha acha kwa dakika 30 au lala nayo halafu asubuhi utaosha kichwa chako.

Fanya zoezi hilo kwa miezi michache tu na utaona matokeo ya nywele zako kila mtu anaweza kukusahau

Kwa ushauri zaidi au maelezo ya kina usisite kutupigia simu kwa namba 0716 300 200/ 0784 300 300/0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment