Wednesday, 28 June 2017

Njia 2 asili za kuondoa hali ya wekundu mashavuni


Kuna baadhi ya wanawake (hasa weupe) ngozi zao za usoni huharibika na kuwa nyekundu hasa maeneo ya mashavuni kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na matumizi ya vipodozi holela.

Hali hiyo ya wekundu kwenye sura hasa maeneo ya mashavuni huchangia mhusika kupoteza muonekano wake halisi na kutovutia.

Leo ninazo mbinu mbili asili za kuondoa hali hiyo ya wekundu usoni kwenye mashavu.

1. Tango

Tango linauwezo wa kusaidia kutatua matatizo kadhaa ya ngozi kutokana na kuwa na vitamin C na madini mbalimbali ambayo huiacha ngozi vizuri pamoja na kuisafisha.

Unachopaswa kufanya ni kukata vipande vya tango kisha tumia vipande hivyo kusugua taratibu sehemu ya ngozi iliyoathirika . Fanya zoezi asubuhi na jioni kila siku hadi pale utakapoona mabadiliko.

2. Mafuta ya nazi

Mtu aliyeathirika ngozi na kuwa na wekundu usiovutia anaweza kutumia mafuta ya nazi halisi na sio ya dukani kwa kupaka taratibu sehemu yenye matatizo asubuhi na jioni angalau kwa mwezi mmoja mfululizo na anauwezo wa kuanza kupata ahueni bila shaka.

Zingatia.
Ili kuepuka na matatizo kama haya ya ngozi ambayo baadaye huweza kusababisha madhara makubwa zaidi ikiwa ni pamoja na saratani ya ngozi ni vyema kuhakikisha unatumia vipodozi vilivyoidhinishwa na mamlaka husika za nchi, lakini pia na kuzingatia ushauri wa wataalam wa afya ya ngozi kabla ya kutumia kitu chochote kwenye ngozi yako.

Unaweza kuuliza maswali mbalimbali kwa kupiga simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.


No comments:

Post a Comment