Tuesday, 27 June 2017

Njia 2 asili za kutuliza maumivu ya tumbo haraka


Kuna wakati unaweza kujikuta umepatwa na maumivu ya tumbo ghafla kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na vyakula.


Maumivu ya tumbo huweza kuchangiwa na ulaji wa vyakula vibichi au vilivyoandaliwa katika mazingira yasiyo safi.

Pia unaweza kupatwa maumivu ya tumbo endapo utakula chakula bila kunawa mikono.

Sasa leo ninazo njia mbili za kupunguza madhara ya maumivu ya tumbo yanayojitokeza ghafla na si kwa sababu ya tumbo la period kwa wanawake wala kwa vidonda vya tumbo.

Njia ya kwanza ni kutumia maji ya uvuguvugu yenye mchanganyiko wa limao. unapohisi maumivu ya tumbo ya ghafla unashauriwa kuandaa maji yenye uvuguvugu na kukamulia kiasi cha limao moja kisha kunywa maji hayo kiasi cha glasi moja pekee.

Njia ya pili unaweza kutumia tangawizi, unachotakiwa kufanya ni kusaga tangawizi yako kisha weka kwenye maji kiasi cha glasi moja halafu weka kwenye moto yachemke kwa dakika tatu kisha kunywa na itaweza kukusaidia kutuliza maumivu hayo ya tumbo.

ZINGATIA
Njia hizi mbili hazitumiki kwa wale wenye tatizo la vidonda vya tumbo bali zinatakiwa kutumiwa na wale wanaopatwa na maumivu hayo ya tumbo ghafla.

Unaweza kuuliza maswali mbalimbali kwa kupiga simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment