Tuesday, 27 June 2017

Njia 3 asili za kupunguza madhara ya U.T.I


Tatizo la kupata haja ndogo (mkojo) yenye kuambata na maumivu makali, huku ikitoka kwa taabu sana hili ni tatizo ambalo huwakumba watu wengi na baadhi yao hushindwa kuelewa sababu ya tatizo hilo.

Kimsingi ni kwamba kupata maumivu wakati wa haja ndogo ni moja ya dalili kuwa mhusika amepatwa na maambukizo kwenye njia ya mkojo (U.T.I) .

Watu wenye tatizo hili hujikuta wakikosa raha na amani kabisa wakati wanapohitaji kupata haja ndogo na wengine hufika wakati kutotamani kabisa kupata haja ndogo.

Hapa ninazo njia tatu ambazo huweza kutoa ahueni kwa mtu mwenye shida ya U.T.I

1. Ulaji wa tango.
Tango lina nafasi  ya kutoa ahueni kwa wale wenye shida ya U.T.I unachotakiwa kufanya ni kutafuna vipande vya tunda hilo vitatu hadi vinne kwa siku asubuhi na jioni hadi utakapoona mabadiliko.

2. Unywaji wa tangawizi
Mtu mwenye shida ya tatizo la mkojo mchafu anaweza pia kupata ahueni endapo atatumia tangawizi kama kinywaji unachotakiwa kufanya ni kusaga tangawizi kisha chemsha pamoja na maji halafu kunywa kikombe kimoja cha kinywaji hicho kutwa mara mbili.

3. Kunywa maji mengi
Hii ni njia nyingine rahisi ya kuwasaidai wenye tatizo la U.T.I kwani wapokunywa maji mengi huwasaidia kupata haja ndogo mara kwa mara na hivyo kuwa moja ya njia ya kutoa bakteria wa ugonjwa huo mwilini na kupunguza madhara ya tatizo.

Unaweza kuongea nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 kama utakuwa na swali lolote au unahitaji ushauri wa kiafya hasa kuhusu lishe bora.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment