Wednesday, 28 June 2017

Njia 3 asili za kutuliza kikohozi

Kikohozi kinaweza kusababishwa na kichocheo cha ndani ya koo, mabadiliko ya hewa au majira, kuziba kwa mifereji ya mapafu n.k

Mara zote unapokooa tambua kuwa lengo kuu hapo huwa ni kutoa chembechembe zisizohitajika katika njia ya kupitisha hewa, lakini kikohozi cha kawaida huweza kupona bila mhusika kutumia dawa ya aina yoyote.

Vifuatavyo ni baadhi ya vitu vinavyopatikana nyumbani na huweza kusaidia kutuliza kukohozi.

1. Tangawizi
Chemsha kikombe kimoja cha tangawizi kisha kunywa asubuhi na jioni kwa siku tatu na itakusaidia.

2. Asali
Pata asali kiasi cha kijiko kimoja cha asali weka na kiwango kidogo cha matone kadhaa ya limao kisha kunywa asubuhi na jioni itakusaidia.

3. Kitunguu maji
Chukua vitunguu maji kisha vikate vipande vidogovidogo halafu changanya na asali kijiko kimoja kisha utatumia mchanganyiko huo.

Zingatia
Mara zote ni muhimu kujua chanzo cha kikohozi chako kabla ya kukimbilia kutumia aina yoyote ya njia ya matibabu, hivyo tunashauri kuwaona wataalam kabla ya kufanya maamuzi ya kutumia chochote .

Pia unaweza kutupigia kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment