Saturday, 17 June 2017

Njia 4 asili za kumaliza tatizo la kipandauso


Kipandauso ni tatizo linalotambulika kwa kusababisha maumivu makali ya kichwa kwa mhusika ambayo mara nyingi hujirudiarudia.

Maumivu haya huweza kuambatana na dalili kadhaa ikiwa ni pamoja na kichefuchefu na hata kutapika.

Tatizo hili mara nyingi huelezwa kutokea kutokana na mchanganyiko wa kimazingira au kiwango cha homini kutokana na kupanda au kushuka.

Matibabu ya awali ambayo hupendekezwa kwa wenye tatizo hili la kipandauso ni pamoja na kutumia dawa zenye kutuliza maumivu.

Hata hivyo, sisi Mandai Products wataalam na waandaaji wa lishe zitokanazo na mimea asili, matunda na viungo tunapenda kukueleza mbinu 4 nyingine zinazoweza kumsaidia mtu mwenye shida ya kipandauso kama huduma ya kwanza.

1. Tangawizi
Kiungo hiki huweza kutoa msaada kwa mwenye tatizo hilo endapo atakunywa chai itokanayo na tangawizi.

Au mhusika naweza kutafuna kipande cha tangawizi na kusaidia kumaliza tatizo hilo au kupunguza dalili za kipandauso.

2. Apple
Tunda hili nalo hufaa kwa mtu mwenye tatizo la kipandauso unaweza kunywa juisi yake halisi au tunda lenyewe na kupata ahueni ya tatizo hilo.

3.Kahawa
Unaweza kunywa kikombe kimoja kidogo cha kahawa na kusaidika kupunguza tatizo hilo.

Zingatia: Matumizi ya kupitiliza ya kahawa huweza pia kuwa na madhara kwa mtu mwenye tatizo hilo.

4. Kuchua kichwa/ massage
Hii inatakiwa kufanywa na mtaalam wa masuala hayo ya massage kama utaona hauna mtu mwenye utaalam wa kutoa huduma hiyo ya massage ni vyema ukatumia hizo mbinu nyingine kwani hii huhitaji umakini mkubwa na utaalam pia katika kazi hiyo.

Usipate shida kujua wapi unaweza kuuliza maswala mbalimbali kuhusu afya yako hasa masuala ya lishe bora na undaaji wake, fanya uamuzi wa kutupigia sasa kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment