Thursday, 8 June 2017

Njia 5 za asili za kuondoa weusi kwenye vifundo vya miguu & mikono


Weusi unapokithiri zaidi kwenye vifundo vya miguu na mikono huweza kutia dosari ya mhusika hasa kwa wanawake na kusababisha hata baadhi ya mavazi kushindwa kuyavaa au kukosa amani wanapoyavaa.

Sasa leo naomba nikwambie baadhi ya njia asili za kumaliza tatizo la weusi uliokithiri kwenye ngozi ya vifundo vya miguu na mikono.

1. Mafuta ya nazi
Unachotakiwa kufanya ni kupata mafuta halisi ya nazi kisha paka kwenye vifundo vya miguu na mikono na usugue taratibu kwa dakika 1 hadi mbili. Fanya zoezi hilo kila siku hadi utakapoona mabadiliko.

2. Limao
Andaa kiasi fulani cha juisi ya limao kisha paka sehemu za vifundo vya miguu na mikono zenye weusi uliokithiri kisha acha kwa dakika 20 kabla ya kunawa sehemu hizo. Zoezi hilo utalifanya hadi utakapoona mabadiliko au kulithika na matokeo.

3. Sukari & Mafuta ya mzaituni
Pata kiasi cha sukari kisha changanya na mafuta ya mzaituni halafu tumia mchanganyiko huo kupaka sehemu yenye tatizo yaani weusi, sugua kwa dakika 5 bila kutumia nguvu sana. Fanya zoezi hili kwa wiki nzima asubuhi na jioni.

4. Aloe Vera
Pata jani fresh la aloe vera na utumie yale majimaji yake kupaka sehemu yenye tatizo hilo, fanya mara moja au mbili kila siku kwa wiki nzima mfululizo.

5. Tango
Kata vipande vidogo vya tunda hili kisha chukua kimoja kimoja na kusugulia polepole kwenye sehemue yenye tatizo hilo la weusi wa ngozi.

Kwa maelezo na ufafanuzi zaidi tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment