Monday, 19 June 2017

Njia 7 rahisi za kupambana na hasira

Kwa hali ya kawaida kila mtu hukasirika pale anapochukizwa au kukasirishwa na jambo fulani, hali hii huweza kumtokea mtu yeyote.


Endapo utaruhusu hasira zikutawale katika maisha yako basi zitakupelekea kuvuruga akili yako na hatimaye kudhoofisha afya yako.

Kimsingi hasira si kitu kizuri kabisa, hasira inaweza kuwa ni ya kubomoa au kujenga, lakini mara nyingi hasira husababisha hasara kwa kuwa inabomoa na kuharibu mambo.

Njia hizi zifuatazo huenda zitaweza kukusaidia katika kutuliza hasira zako

Kwanza penda kufikiri kabla hujaongea

Pale unapohisi unashindwa unahasira. Ni vyema ukakaa kimya au kuondoka kabisa mahali ulipo ili kuepusha kuongea mambo ambayo yatakufanya ujute hapo baadae. Utakapo kaa kimya ni rahisi hata kwa mtu/watu unaongea nao kutulia kwakuwa hutoonyesha dalili ya kutaka kujibizana

Ikiwa mtu atakulazimisha kwa namna moja au nyingine uongee basi ni vyema ukamwambia sipo tayari kuongea na wewe kwa sasa labda baadae na ondoka katika eneo hilo bila kusema neno lingine lolote.

Vuta pumzi

Unapokuwa na hasira, mapigo ya moyo nayo huongezeka kwa kasi, halikadhalika nguvu nazo zinaongezeka na mwili unakuwa tayari kufanya lolote pasipo kufikiri.

Unapofikia hatua hiyo huwa ni mbaya sana kwani chochote huweza kutokea na ikawa hatari zaidi.

Hali hiyo inapaswa kudhibitiwa na wewe mwenyewe kabla hujakuwa na hasira zaidi. Itakubidi ushushe hasira zako kwa kukaa chini na kutulia kisha vuta pumzi, jitahidi kuhimili mihemko yako ya mwili kwa kutofanya lolote bali kutulia na kuvuta pumzi na kupumua angalau kwa dakika 5. Jitahidi kuvuta pumzi ndani taratibu na kwa wingi kisha pumua. Baada ya dakika 2-3 bila shaka utaanza kujisikia mwenye amani.

Tafuta sehemu yenye amani
Pale unapohisi unahasira ni vyema ukaenda mahali ambapo unaweza kupata furaha mfano bustanini kwenye majani na maua mazuri au kwenye fukwe za bahari au ziwa (beach), na pengine popote pale ambapo unaweza ukaondoa mawazo mabaya na kujifariji.


Washirikishe watu unaowaamini shida yako.


Kueleza mambo yanayokusibu kwa mtu mwingine ni njia nzuri ya kutoa kero zako zinazokufanya ukasirike.

Mtu wako wa karibu anaweza kuwa mzazi, mmeo, mkeo, kaka au jamaa yako wako wa karibu. Ikiwa utaeleza kero zako kwa mtu wako wa karibu utatoa yaliyo moyoni mwako na kuwa mwenye amani.

Pia utakapomueleza mtu yanayokusibu ni rahisi kupata ushauri mzuri kutoka kwake ambao huenda utakusaidia kutatua tatizo lako.

Kaa mbali na kitu au mtu anayekufanya kuchukia.
Huenda hasira zako hutokea baada ya kumuona mtu fulani au kitu fulani usichokipenda. Hivyo hakikisha unakaa mbali na chochote kinachokufanya ukasirike.

Ikiwa ni mtu fulani ndiye anakusababisha ukasirike ni vyema ukatafuta ufumbuzi wa mgogoro wenu na kuweka mambo sawa.

Hesabu namba kichwani 1 mpaka 20

Mbinu hii inaweza kuonekana kama haina mashiko wala haina faida katika kutatua tatizo hili, lakini ikiwa utaitumia itakusaidia kuondoa mawazo ya kitu au mtu aliyekukasirisha na kuweza kujimudu kupambana na hasira zako.

Tulia na uvute pumzi na kisha pumua taratibu, anza kuhesabu namba kuanzia 1 kupanda mpaka 20 bila kufikiri chochote isipokuwa weka mawazo yako katika kuhesabu namba.

Usiruhusu mtu akukatishe hivyo itabidi ukae mahali peke yako au ikiwezekana tulia na hesabu namba zako bila kusikiliza chochote.

Fanya zoezi lolote la kuchangamsha mwili

Jishughulishe na mchezo wowote au mazoezi kama kukimbia angalau kilomita 2 au tembea kwa miguu kwa umbali Fulani pia unaweza kuendesha baiskeli.

Lengo la mazoezi hayo ni kubadilii mazingira, kufikiri na kuona mengine kuliko kukaa sehemu moja na kufikiri mambo hayo hayo yanayokusabibisha upate hasira.

Unaweza pia kupokea ushauri wa bure kutoka kwetu kuhusu masuala ya lishe bora tupigie sasa kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com tupo kwaajili yako karibu.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment