Thursday, 15 June 2017

Njia asili ya kupunguza tatizo la kutokwa na ute mweupe sehemu za siriKutokwa na majimaji meupe yasiyo na rangi wala harufu mbaya katika sehemu za siri za kike, ni jambo la kawaida kwa wasichana na wanawake wenye afya.


Ila majimaji hayo yakiwa mengi sana kiasi cha kuchilizika mapajani na kulowanisha kabisa nguo za ndani, hali hiyo yaweza kuwa si ya kawaida. Au maji hayo yakiwa yanayowasha au kuwa na harufu mbaya au yaliyoganda kama maziwa ya mgando hilo huweza kuwa tatizo la uambukizo fangasi au magonjwa ya zinaa kama vile kisonono.

Uwepo wa unyevunyevu sehemu za siri kwa muda mrefu huweza kusababisha harufu mbaya kutokana na kushambuliwa na bakteria wanaokaa na kuzaliana kwenye ngozi. Harufu ambayo husababisha usumbufu kwa mhusika, lakini pia na watu wake wengine wa karibu.

Hali huweza kupunguzwa au kumalizwa kwa msichana kunawa mara kwa mara kwa maji na sabuni isiyokuwa na kemikali kali na kujikausha kwa kitambaa safi cha nguo ya pamba.

Aidha wataalam wa afya wanaeleza kuwa mwanamke anaweza kupunguza madhara ya tatizo hilo kwa kuvaa nguo za ndani zenye uwezo wa kunyonya unyevunyevu hasa zile zenye asili ya pamba au zinazopitisha hewa kupitia matundu madogo madogo.

Pamoja na hayo, msichana mwenye tatizo hili anashauriwa kutumia juisi yenye mchanganyiko wa matunda mbalimbali angalau kwa wiki tatu mfululizo hali ambayo husaidia kuimarisha kinga za mwili na kupambana na maambukizi hayo.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0769 400 800, 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment