Friday, 30 June 2017

Orodha ya vyakula 5 vinavyoweza kukuepusha na matatizo ya figo

AFYA ya figo ni muhimu, hii ni kwa sababu figo ni moja ya kiungo ambacho husaidia kuchuja sumu mbalimbali ndani ya mwili na baadaye kutoa taka mwili kwa njia ya haja ndogo (mkojo)

Matatizo ya figo huweza kuchangia ugumu wa upatikanaji wa haja ndogo (mkojo) au miguu na mikono kuvimba.

Pia mtu mwenye shida ya figo huwa katika hatari ya kukumbwa na matatizo ya moyo.

Hata hivyo, kuna baadhi ya vyakula na vinywaji ambavyo tunaweza kusema ni vyakula rafiki kwa afya ya figo ndani ya mwili na husaidia kulinda afya kiungo hicho.

1. Matumizi ya juisi
Juisi mbalimbali za matunda nazo zinauwezo mzuri wa kulinda afya ya figo, miongoni mwa matunda ambayo yanashauriwa kutumika katika kulinda afya ya figo ni pamoja na 'apple', nanasi, tango, chungwa pamoja na peazi.

2. Mboga za majani
Mboga za majani pia husaidia kulinda afya ya figo, mfano wa mboga hizo ni pamoja na spinachi

3. Kunywa maji ya kutosha
Unywaji wa maji ya kutosha mara kwa mara ni moja ya njia ya kulinda afya ya figo yako, hivyo ni vizuri kuzingatia kunywa maji ya kutosha kila siku angalau yasiyopungua glasi 8.

4. Maji ya dafu
Hii nayo ni njia nyingine muhimu kwa wale wenye nia ya kulinda afya ya figo kwani maji hayo husaidia kuboresha afya figo ikiwa ni pamoja na kuweka mbali tatizo la mawe kwenye figo.

5. Kitunguu maji
Kitunguu maji kinapochemshwa pia husaidia kukinga figo dhidi ya tatizo la mawe, unachopaswa kufanya ni kuchemsha maji glasi yakiwa na vitunguu viwili hadi vitatu kama ni vidogo na uache vichemke kwa dakika kumi na tano.

Baada ya hapo changanya vizuri na uache mchanganyiko huo upoe. Baada ya hapo kuna vitu viwili vya kuongeza kwenye mchanganyiko huo kabla ya kunywa. Sasa ili kufahamu vitu hivyo viwili piga simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com tutakupatia ufafanuzi.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment