Friday, 16 June 2017

Pilipili manga inatumika sana wakati huu wa mfungo, zifahamu faida zake 4 za kiungo hicho

PILIPILI manga ni mbegu ndogo ndogo ambazo ukiziangalia vizuri sana basi zinataka kufanana na mbegu za papai.

Rangi yake ni nyeusi hivi na ladha yake ni mfano wa pilipili.

Moja ya faida za kiungo hiki ni pamoja na kuwasaidia wale wenye matatizo ya upumuaji na kuongeza hamu ya kula, hivyo ni kiungo kizuri sana kwa wale wenye kukosa hamu ya chakula.

Aidha, pilipili manga pia inaelezwa kutoa ahueni kwa wenye matatizo ya tumbo pamoja na kusaidia kwa wale wenye tatizo la kuhara.

Kazi nyingine ya kiungo hiki mwilini ni pamoja na kupunguza uzito kwa wenye shida ya uzito mkubwa sambamba na kuboresha afya ya ngozi na kuifanya kuonekana vyema zaidi.

Mbali na hayo, kiungo hiki kuna wakati kinapotumika vizuri huweza kutoa ahueni kwa wenye tatizo la vidonda vya tumbo kutokana na kuwa antioxidants pamoja anti-inflammatory.

Zingatia.
Matumizi ya pilipili manga huweza kumsababishia mtumiaji kupiga chafya pia si nzuri kwa waliotoka kufanyiwa uparesheni hasa wa tumbo.

Kwa maelezo zaidi kuhusu mada hii na nyingine nyingi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment