Monday, 5 June 2017

Pokea faida za majani ya nanasi leo


Habari za Jumatatu mpendwa mfuatiliaji wetu wa www.dkmandai.com leo ni siku nzuri tena ambapo tunaendelea kufahamishana kuhusu mimea tiba mbalimbali.

Ndani ya weekend hii nashukuru sana kwani nimepokea maswali mengi sana kupitia namba ya simu ya 0769 400 800 ambapo wengi waliuliza kwanini tumekuwa tukizungumzia sana faida za nanasi kama tunda na juisi yake, lakini hatujawahi kuongelea kabisa kuhusu yale majani yake?

Hivyo nimeona nitumie nafasi hii kuwajibu wale wengi waliohitaji kujua faida za majani ya mnanasi.

Kama umekuwa ukifuatilia tovuti hii naamini utakuwa unafahamu kwamba mara kadhaa tumeshazungumzia umuhimu wa matumizi ya tunda la nanasi kiafya.

Lakini leo tunakufahamisha matumizi ya majani au matawi ya mmea wenyewe wa nanasi.

Majani haya yanauwezo wa kuwasaidia sana wale wenye matatizo ya figo, kujaa kwa miguu au miguu kuwaka moto na kupasuka.

Majani haya pia yanauwezo wa kuwasaidia wale wenye shida ya kuumwa na kichwa mara kwa mara.

Unachopaswa kufanya ili majani haya yawe msaada kwako kama tiba ni kuhakikisaha unapata majani matano ya mmea huu wa nanasi kisha yasage na kuchanganya kwenye maji ya moto na baadaye chuja.

Baada ya hapo subiri maji hayo yenye mchanganyiko wa majani ya nanasi yapoe kisha mhusika yaani mgonjwa atumie kiasi cha nusu glasi asubuhi na jioni.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment