Tuesday, 27 June 2017

Sababu 5 zinazosababisha maumivu ya kichwa asubuhiJe, kuna baadhi ya siku umejikuta ukiamka asubuhi ukiwa na maumivu ya kichwa kwa mbali na kukufanya kutojisikia vizuri na hata kudhani huenda unaumwa?

Sasa leo naomba nikwambie  baadhi ya sababu ambazo huweza kupelekea mtu kuamka asubuhi akiwa na maumivu ya kichwa.

1. Haukulala kiasi cha kutosha
Mwili wako unahitaji saa saba hadi nene kupumzika usiku kwahiyo unapolala chini ya masaa hayo huweza kusababisha kupatwa na maumivu hayo ya kichwa wakati wa asubuhi unapoamka.

2. Umelala kupita kiasi
Pia unapolala sana kupitiliza zaidi ya saa saba hadi nane huweza kuchangia maumivu ya kichwa wakati wa kuamka asubuhi.

3. Ulikunywa pombe sana kabla ya kulala.
Unapokunywa vileo kabla ya kulala usiku nayo huweza kuwa sababu ya kuchangia maumivu ya kichwa wakati wa asubuhi, hivyo ni vyema kupunguza unywaji wa pombe kupita kiasi au kuacha kabisa ikibidi.

4. Unakoloma sana usiku
Unapoona kila unapoamka asubuhi na unajikuta unamaumivu ya kichwa tambua kuwa huenda usiku huwa unakoloma sana, hivyo asubuhi unakuwa umechoka na huweza kuchangia kupatwa na maumivu hayo ya kichwa.

5. Unamsongo wa mawazo
Unapozongwa na kiwango kikubwa cha mawazo hasa usiku kabla ya kulala ukifikiria mambo mengi tambua kuwa itakuwa ni rahisi kwako kuamka asubuhi ukisindikizwa na maumivu ya kichwa, hivyo ni vyema kupunguza msongo wa mawazo au kuwaona wataalam wa saikolojia kwa ushauri zaidi.

Unaweza kuongea nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 kama utakuwa na swali lolote au unahitaji ushauri wa kiafya hasa kuhusu lishe bora.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment