Tuesday, 6 June 2017

Sababu za miguu kuvimba na jinsi kitunguu maji kinavyoweza kumaliza tatizo hilo


Hivi ni mara ngapi umesikia mtu akilalamika kuwa miguu imejaa maji au imevimba? Inawezekana hiyo hali imewahi kukutokea wewe mwenyewe au inawezekana likawa ni moja la tatizo ambalo hadi sasa linakusaumbua au linamsumbua mtu wako wa karibu.

Sasa leo kupitia tovuti yako hii pendwa ya www.dkmandai.com nimeona nikueleze baadhi ya mbinu asili  za kutatua tatizo hilo.

Kwanza kabisa ifahamike kuwa tatizo hilo huweza kuchangiwa na ongezeko la juu la madini ya sodium mwilini au uwepo wa mzunguko hafifu wa damu ndani ya mwili.

Pia tatizo hilo huchangiwa na ukosefu wa mazoezi, upungufu wa vitamin fulanifulani , lakini pia hali hiyo huweza kuwakuta kinamama wajawazito na hata baadhi ya wanawake wanapokaribia kuingia kwenye period zao.

Sababu nyingine za tatizo hili ni pamoja na hali ya joto kali na baadhi ya magonjwa kama shinikizo la damu, matatizo ya moyo, matatizo ya figo, ugonjwa wa ini, ugonjwa sugu wa mapafu na wakati mwiingine hata matumizi holela ya baadhi ya dawa huweza kuchangia tatizo hili la miguu kuvimba au kujaa maji.

Namna ya kumaliza tatizo hili kwa njia asili

1. Maji ya uvuguvugu & chumvi

Unachotakiwa kufanya ni kuandaa beseni lenye maji ya uvuguvugu kisha weka kijiko kimoja cha chakula chenye chumvi ndani ya maji hayo, halafu weka miguu yako ndani ya mchanganyiko huo kwa dakika 15 hadi 20.

Baada ya hapo utaitoa na kuikausha vizuri kwa taulo safi. Fanya hivyo mara 3 hadi 4 kwa siku ndani ya wiki moja hadi mbili mfululizo.

2.Kitunguu maji

Chemsha vitunguu vyako kadhaa kwenye sufuria yenye maji kiasi cha vikombe vinne na baada ya hapo weka chumvi kidogo. Kisha tumia mchangayiko huo kunywa asubuhi kikombe kimoja na jioni kikombe kimoja kwa wiki moja hadi mbili mfululizo.

Kwa ufafanuzi zaidi wasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com


Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha
tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment