Wednesday, 21 June 2017

Tabia 5 zinazoweza kuchangia mwanamke kushindwa kushika mimba


Kuna baadhi ya wanawake hujikuta wakiingia kwenye tatizo la kutoshika ujauzito kwa mda mrefu bila kutambua sababu kuu ni ipi.

Leo ninazo baadhi ya sababu ambazo nazo huweza kuwa miongoni mwa sababu za kuchangia mwanamke kushindwa kushika ujauzito kwa kipindi fulani.

1. Unywaji wa kupindukia wa vinywaji vyenye caffeine 
Vinywaji vyenye caffaine ni pamoja na kahawa, chai ya rangi vinywaji hivi vinapotumika kupindukia huweza kuwa na madhara kwa mama anayrhitaji kushika ujauzito na mara nyingine hata kwa mama ambaye tayari ni mjamzito.

2. Ufanyaji wa mazoezi kupitiliza
Mazoezi ni muhimu kwa mwanamke, lakini hayapaswi kuzidi kiwango yanapopitiliza huweza kuwa na madhara fulani fulani ikiwa ni pamoja na hili la kutoshindwa kushika ujauzito.

3. Unywaji wa pombe/ vileo
Unapohitaji kushika ujauzito kirahisi ni vyema kupunguza au kuacha kabisa matumizi ya pombe.

4. Matumizi ya Sigara
Wanawake wanaotumia sigara huweza kuwa na madhara ya kiafya ikiwa ni pamoja na kushindwa kushika ujauzito wakati fulani fulani.

5. Kushiriki mapenzi salama
Ukiwa kama mwanamke lazima uzingatie kushiriki penzi salama ili kuepuka magonjwa mbalimbali hasa ya zinaa kwani magonjwa hayo huweza kuchangia ugumu katika kushika ujauzito.

Unaweza pia kupokea ushauri wa bure kutoka kwetu kuhusu masuala ya lishe bora tupigie sasa kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com tupo kwaajili yako karibu.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila sikuNo comments:

Post a Comment