Saturday, 10 June 2017

Tabia 5 zitakazoimarisha kinga zako za mwili

Uimara wa kinga za mwili kwa binadamu ni muhimu sana katika maisha kwani husaidia kumfanya mwanadamu kutozongwa na magonjwa ya hapa na pale na hivyo kuishi akiwa na afya njema.

Kimsingi kinga za mwili huweza kupanda au kushuka kutokana na aina ya vyakula mhusika anavyokula au vinywaji unavyokunywa, lakini pia hata mtindo mzima wa maisha ya mhusika.

Hivyo leo nimeona nikwambie msomaji wangu kuhusu aina za tabia ambazo zitakufanya uendelee kuwa na kinga za mwili imara zaidi.

1. Jenga utamaduni wa kuzingatia usafi, ikiwa ni pamoja na kunawa kabla ya kula na kila baada ya kutoka chooni na hata kuosha matunda na vyakula mbalimbali

2.Jenga tabia ya kunywa maji mengi kila siku, hii husaidia kupunguza sumu mwilini kupitia jasho na haja ndogo na hivyo kuzipunguzia kinga zako za mwili kazi zaidi.

3. Jenga utamaduni wa kufurahi na kucheka pale inapobidi, diyo siku zote kuishi ukiwa na msongo wa mawazo na bila furaha hii huchangia kuharibu kinga zako za mwili na hivyo kuwa rahisi kwako kushambuliwa na magonjwa mbalimbali.

4. Mara zote anza siku yako vyema kwa furaha na kuandaa kifungua kinywa unachokipenda.

5. Kuwa na utamaduni wa kufanya mazoezi ya kutembea kila siku, kwani hii ni moja ya mbinu ya kuimarisha kinga zako za mwili.

Kwa maelezo zaidi tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Kumbuka kwamba dondoo hizi zimeletwa kwenu chini ya udhamini wa The Work Up Tanzania shirika lisilokuwa la kiserikali lenye dhamira ya dhati ya kumbana na umasikini ujinga na maradhi. Tunapatikana Ukonga, Mongolandege zilipokuwa ofisi za Mandai Herbalist Clinic zamani.


No comments:

Post a Comment