Thursday, 22 June 2017

Tatizo 1 ambalo huweza kuchangia mwanamke kuwa mgumba


Hali ya kujaa maji kwenye mirija ya uzazi ya wanawake ni miongoni mwa matatizo ambayo huweza kuchangia mwanamke kuingia kwenye tatizo la kushindwa kushika ujauzito 'ugumba'

Tatizo hili pia  huitwa hydrosalpinx kwa lugha ya kitaalamu ni tatizo ambalo hujitokeza kwa wanawake kutokana na maambukizi ya magonjwa ya zinaa yasiyotibiwa.

Sababu nyingine za tatizo hili

1.  Maambukizi ya magonjwa ya zinaa ambayo hushindwa kutibiwa kwa muda mrefu.

2. Upasuaji maeneo ya kiunoni (pelvic surgery)

3. Endometriosis

4. Saratani ya mirija ya uzazi

Mara nyingi wanawake wenye tatizo hili huwa si rahisi kwao kuhisi dalili zozote, lakini kunawakati huweza kuhisi maumivu ya kiuno au kuwa  na historia ya kutopata mtoto kwa muda mrefu.

Zingatia
Unapohisi kuwa na tatizo hilo ni vyema kufika kwenye hospitali iliyokaribu nawe kwaajili ya uchunguzi zaidi wa kiafya ili kuweza kupatiwa matibabu ya haraka.

Tupo tayari kutoa ushauri kwako pia kuhusu lishe bora na afya yako kwa ujumla unaweza kutuuliza chochote kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment