Thursday, 15 June 2017

Vitu 3 kwa wanaume wenye tatizo la uzalishaji wa mbegu

Mara nyingi familia au ndoa nyingi zinapokumbwa na tatizo la kukosa watoto lawama nyingi huelekezwa zaidi kwa wanawake jambo ambalo si sahihi sana kwani kuna wakati tatizo hilo huweza kuchangiwa na kinababa pia.

Ni vyema ikafahamika kwamba wanaume nao huweza kuwa sababu ya matatizo ya uzazi au kutopata mtoto ndani ya familia.

Miongoni mwa sababu ambazo huchangia tatizo kwa wanaume ni pamoja na kutokuwa na kiwango cha kuridhisha cha mbegu au mbegu kutokuwa na virutubisho vya kusababisha ujamzito.

Leo hapa ninavyo vitu vitatu ambavyo husaidia kuboresha afya ya mbegu za kiume.

1. Komamanga
Unapokula tunda la komamanga au kunywa juisi yake mara kwa mara ambayo husaidia kuongeza wingi wa mani. Hii ni kwasababu tunda hilo lina kitu kiitwacho antioxidants pia juisi ya tunda hilo husaidia kufanya manii kutembea kwa kasi pia.

2. Ndizi
Ndizi ni tunda nzuri ambalo huongeza wingi wa manii pia, Tunda hili ndani yake kuna bromelain ambayo huenda kusaidia mihemko pia ya tendo la ndoa.

Pamoja na hayo, tunda hili lina vitamin A, B1, C vitamin zote hizo husaidia kuimarisha manii.

3. Kitunguu Swaumu
Kiungo hiki kina kitu kiitwacho allicin ambayo pia huchangia kuboresha mzunguko wa damu ndani ya mwili pamoja na kuimarisha afya ya manii.

Pamoja na kuzingatia matumizi ya vitu hivyo kumbuka kuwa mazoezi nayo ni muhimu pamoja na kuepuka msongo wa mawazo na unywaji wa vileo .

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa simu namba +255 716 300 200, +255 769 400 800, +255 784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment