Tuesday, 27 June 2017

Vitu 7 vitakavyokuepusha na kisukari kama ukizingatia


Ugonjwa wa kisukari ni moja ya magonjwa yasiyoambukiza, ambayo husababishwa baada ya kongosho kushindwa kutengeneza 'insulin' ya kutosha ndani ya mwili.

Insulin ni homoni ambayo kazi yake kubwa ndani ya mwili ni kurekebisha kiwango cha sukari kwenye damu.

Sasa Jumamosi ya leo naomba nikwambie wewe msomaji wangu haya mambo saba ambayo ukiyafanya kila siku unaweza kujiweka mbali na ugonjwa huu wa kisukari.

1. Kuwa na uzito wa kawaida
Zingatia kuwa na uzito unaoendana na wewe kiafya kwani hali ya uzito mkubwa huweza kuwa chanzo cha tatizo hili la kisukari. Unapokuwa na uzito wa kawaida unaambiwa kuwa utakuwa umejiweka mbali na ugonjwa wa kisukari kwa asilimia 6.

2. Zingatia ulaji bora
Unapaswa kula chakula kwa kufuata taratibu bora za kiafya ikiwa ni pamoja na kuzingatia ulaji wa matunda pamoja na mbogamboga.

3. Kunywa maji ya kutosha

Unashauriwa kunywa maji ya kutosha kadri uwezavyo, unatakiwa kunywa angalau glass 7 hadi 8 kwa kila siku

4. Usisahau kufanya mazoezi
Mazoezi ni muhimu kwa kila mtu, hivyo kama wewe unapenda kuepukana na ugonjwa huu wa kisukari ni vyema kujitahidi kunywa maji ya kutosha kila siku.

5. Epuka msongo wa mawazo
Mawazo nayo yanapozidi huweza kuwa chanzo cha tatizo hili la kisukari, hivyo jitahidi kuepuka tabia ya kuwa na msongo wa mawazo mara kwa mara ili kujiweka mbali zaidi na ugonjwa wa kisukari.

6.Pata muda wa kutosha wa kulala

Kulala nako ni muhimu kwa afya zetu wanadamu pia ni moja ya njia ya kufanya kuepuka na ugonjwa huu wa kisukari

7. Fanya uchunguzi wa afya mara kwa mara

Jitahidi kujenga utaratibu wa kuchunguza afya yako mara kwa mara ili iwe rahisi kugundua matatizo yako ya kiafya mapema kabla ya tatizo kuwa kubwa zaidi.

Zingatia
Kama ungependa kutuuliza maswali zaidi kuhusu mada hii na hata masuala mengine mengi kuhusu mimea tiba, matunda na lishe bora kwa ujumla wake basi tupigie sasa kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment