Saturday, 3 June 2017

Zipo hapa faida za tunda la mpesheni mwilini

Habari za leo mpenzi msomaji wa tovuti yetu karibu katika muendelezo wa kupeana taarifa kuhusu mimea tiba na afya kwa ujumla.

Leo napenda tuzungumzie mapesheni, tunda hili mmea wake hukuwa kwa kutambaa, hivyo katika ukuaji wake ni muhimu kuweka miti ili iweze kusaidia kukua vizuri.

Mapesheni yanasifika kwa kuwa na virutubisho bora kwa afya ya binadamu ikiwemo vitamin A, C, B2, B6, na E, flavonoids, pectin pamoja na madini ya chuma.

Mpesheni yanauwezo mzuri katika kupunguza maumivu ya mishipa ya fahamu na maumivu ya tumbo la hedhi.

Halikadhalika hali mapesheni husaidia kutibu matatizo ya wasiwasi, msongo wa mawazo na hali ya kuzubaa kwa wazee na watoto.

Zingatia
Hata hivyo, watafiti wanasema kuwa, wajawazito na watoto wachanga wanapaswa kuchukua tahadhari wanapotumia tunda hili, hii ni kutokana na katika majaribio ya utafiti huo walibaini matunda hayo yanauwezo wa kusababisha uchungu na kusababisha watoto kuzaliwa kabla ya wakati, lakini pia huweza kusababisha usingizi hivyo si vizuri kutumiwa na madereva.

Ni vyema kupata maelezo ya kina zaidi kutoka kwetu kabla ya kuanza kutumia matunda haya, wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment