
Sasa hapa ninavyo baadhi ya vyakula ambavyo husaidia kusaidia maziwa kutoka kwa wingi kwa kina mama wanaonyonyesha.
1. Chungwa
Tunda hili huweza kuwa msaada kwa kinamama wanaonyonyesha kutokana na kuwa na vitamin C yakutosha.
2. Uwatu
Uwatu unaweza kutumia mbegu zake au majani yake yote husaidia kuhamasisha mwili wa mwanamke kutengeneza maziwa ya kutosha.
3. Karoti
Karoti inautajiri wa vitamin A ambayo nayo ni muhimu kwa wanawake, lakini mbali na vitamin A, pia kuna kitu kiitwacho alpha na beta carotene ambayo huaminika husaidia kuhamasisha mwili wa mama anayenyonyesha kupata maziwa mengi zaidi.
4. Spinach
Ni miongoni kati ya mbogamboga muhimu ambayo pia imesheheni vitamin A na ni muhimu kwa kinamama wanaotoka kujifungua kutokana na kuongeza damu pia.
Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.
No comments:
Post a Comment