Monday, 31 July 2017

Aina 4 ya vyakula vinavyopunguza tatizo la kukatika kwa nyweleMoja ya vitu ambavyo husaidia kuufanya mwili wa binadamu kuonekana vizuri ni pamoja na nywele, lakini ili nywele zilete mvuto lazima ziwe na muonekano mzuri.

Leo ndio maana nimeona ni vyema tuangazie kuhusu aina ya vyakula na matunda ambavo husaidia kuzuia tatizo la nywele kukatika au kunyonyoka.

Vifuatavyo ni vyakula na matunda ambavyo huweza kusaidia kuzia tatizo hilo:-

1. Mboga za majani
Mboga hizi za majani hususani spinach huweza kuboresha afya ya nywele hasa nywele zinazokatika kutokana na mboga hiyo kuwa na kuwa na vitamin B, C na E pamoja na madini ya potassium na calcium chuma na magnesium ambayo kwa pamoja huhitajika kwa makuzi ya nywele.

2. Mayai
Myai yanasifika kwa kuwa na protini ambayo pia huhitajika kwa afya na makuzi ya nywele. lakini protini inayopatikana kwenye  mayai hufaa zaidi kwa afya ya nywele.

Zingatia upate mayai ya kuku wa kienyeji zaidi ili kunufaika na protini hiyo.

3.Karanga
Hizi nazo zinavirutubisho mbalimbali ambazo husaidia kuhamasisha uotaji wa nywele na hivyo kuepuka tatizo la kukatika hovyo kwa nywele. Hivyo matumizi ya mara kwa mara ya karanga husaidia ukuaji wa nywele.

4. Samaki
Kitoweo hiki ni chanzo kizuri cha omega 3 ambayo ni nzuri kwa ukuaji wa nywele

Kwa ushauri zaidi tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com au fika ofisi zetu Makao makuu Ukonga, Mombasa mtaa wa Mongolandege jijini Dar es Salaam.

Pamoja na hayo, bado unaweza kupakua Application yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment