Tuesday, 25 July 2017

Faida 4 za kuzingatia ulaji wa polepole

Kutokana na pilika pilika za kila siku za kujipatia kipato walizonazo watu wengi kwa sasa  ambazo kuna wakati huwa zinavuruga kabisa hata mpangilio wa mlo. Au kumlazimu mtu kula haraka haraka kwa kuwahi majukumu.

Ni ukweli kuwa kwasasa kuna baadhi ya watu hujikuta hawatulii mezani kabisa wakati wa kula kwa sababu ya kuwa na harakati za kukimbizana na maisha.

Leo napenda tufahamishane huu umuhimu wa kiafya wa kula taratibu na kwa utulivu

1. Ulaji wa utulivu na wapolepole husaidia kuboresha umen'genyaji wa chakula tumboni, hii inamaana kwamba siku zote umeng'enyaji wa chakula huanzia mdomoni hivyo ni muhimu kutafuna taratibu na vizuri chakula ili kurahisisha umeng'enyaji wa chakula kinapofika tumboni.

2. Ulaji wa polepole husaidia kupunguza mawazo 'stress'

3. Ulaji wa polepole husaidia kufurahia chakula na kusikia vizuri 'taste' ya chakula.

4. Husaidia kupunguza uzito, tafiti mbalimbali zinaonesha kuwa ulaji wa polepole husaidia sana mhusika kuwa na uzito mkubwa. Mara nyingi mtu anayekula haraka hujikuta amakula chakula kingi kwa mda mfupi hivyo kama alikuwa anahitaji kuwa na uzito unaokubalika kiafya hujikuta anashindwa.

Kwa ushauri zaidi kuhusu lishe bora unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment