Friday, 28 July 2017

Faida za kiafya za ulaji wa pweza na supu yake

Pweza ni aina ya samaki ambaye anawingi wa virutubisho mbalimbali ambavyo huusaidia mwili kujikinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.

Miongoni mwa magonjwa ambayo huweza kukingwa dhidi ya kitoweo hiki ni pamoja na saratani ya mdomo, utumbo mkubwa, tumbo, matiti, shingo ya kizazi nk.

Aidha kitoweo hiki (Pweza) kimejaa na virutubisho vinavyosaidia kuongeza hamu ya kushiriki tendo la ndoa. Hii ni kutokana na uwepo wa virutubisho aina ya protini na madini ya selenium.

Pia pweza husaidia mwili kufanya kazi zake vizuri ikiwamo mfumo wa mmeng’enyo wa chakula, upumuaji na hata mzunguko wa damu.

Kwa upande wa kina mama, pweza husaidia katika uzalishaji wa maziwa pindi wanapojifungua

Faida nyingine waipatayo watumiaji wa supu ya pweza ni kuongeza madini joto mwilini, lakini pia virutubisho vilivyomo ndani ya pweza husaidia kupunguza athari za maradhi ya moyo kwa kuwepo mafuta ya omega-3 fatty acid.

Zingatia
Kikubwa zingatia hali ya usafi sehemu utakayoamua kula pweza ili kuepuka magonjwa mbalimbali  pia

Unaweza kuwasiliana nasi kwa ushauri zaidi pamoja na maoni kupitia simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe: dkmandaitz@gmail.com

Pamoja na hayo, bado unaweza kupakua Application yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment