Monday, 3 July 2017

Gimbi linafaida zaidi ya kiazi kitamu

Magimbi ni miongoni mwa mazao ambayo hupatikana kwa mfumo wa mizizi. Magimbi hulimwa sehemu mbalimbali hapa nchini hususani maeneo ya mabondeni ambapo maji hupatikana zaidi.

Magimbi yamesheheni virutubisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na vitamini B6, B1, C pamoja na folic acid.

Ulaji wa magimbi husaidia kuimarisha kinga ya mwili kutokana na kuwa na vitamin C, lakini pia chakula hiki kina wingi wa nyuzinyuzi yaani 'fiber' ambayo ni muhimu kwa afya ya mfumo wa umeng'enyaji wa chakula.

Hivyo mtumiaji wa magimbi mara kwa mara huweza kuepeuka tatizo la kutopata choo au kupata choo kwa tabu.

Magimbi yanataka kufanana na viazi vitamu kuhusu virutubisho, lakini magimbi yanaweza kuwa na manufaa zaidi kutokana na kuwa na protini nyingi zaidi kuliko ile inayopatikana ndani ya viazi.

Kwa ufafanuzi zaidi na maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment