Thursday, 13 July 2017

Ifahamu juisi yenye uwezo wa kuondoa tatizo la jasho

Habari za leo mpendwa msomaji wangu wa www.dkmandai.com leo napenda tuzungumze kuhusu tatizo la kutokwa na jasho kupita kiasi.

Kwanza ni vizuri ikafahamika kwamba kutokwa jasho ni njia mojawapo ya mwili kutoa taka, lakini pia ni mfumo unaotumiwa na mwili ili kuupooza pale hali ya hewa au joto la mwili linapokuwa limepanda.

Kila mtu huweza kutokwa na jasho, lakini kwa kawaida mwili hutoa jasho baada ya mtu kufanya shughuli fulani ya kufanya joto la mwili kupanda, lakini pia jasho huweza kutoka endapo mhusika atakumbwa na msisimko fulani, basi hapo pia jasho linaweza kumtoka.

Aidha kuna baadhi ya watu ambao mbali na sababu hizo hapo juu, huweza kujikuta wakitokwa na jsho licha ya kuwa hawajafanya shughuli yoyote wala hawajakumbwa na msisimko wa aina yoyote ile na kitaalam tatizo hilo hufahamika kama 'hyperhidrosis.'

Moja ya mambo ambayo huweza kusaidia kuondoa tatizo hili ni pamoja na unywaji wa juisi ya nyanya endapo itaandaliwa vyema.Juisi hii inavitamin mbalimbali pamoja na madini ya potassium sambamba na vitamin C.

Kwa maelezo zaidi tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment