Friday, 21 July 2017

Ifahamu njia ya kumaliza maumivu ya kiuno haraka


Habari za leo mdau wa tovuti hii, karibu sana tuendelee kuyafahamu mengine zaidi kuhusu afya zetu.

Kumekuwa na maswali mengi nimeendelea kupokea kupitia namba zetu za 0716 300 200, 0769 400 800 na moja ya swali ambalo nimelipokea sana wiki hii ni hili la kuhusu maumivu ya kiuno.

Mara nyingi malalamiko ya kuumwa kiuno huwatokea zaidi kinamama na mabinti, licha ya kwamba mara chache pia huweza kutokea kwa wanaume , lakini sababu kubwa za kuumwa kiuno ni pamoja na hizi zifuatazo:-

1. Unyanyuaji au ubebaji wa mizigo mizito

2. Hali ya kukosa choo kwa muda mrefu

3. Kukaa isivyostahili kwa muda mrefu.

4. Kutokuwa na mazoezi ya kutosha

5. Matatizo katika kipindi cha hedhi

6. Kufanya kazi za kusimama kwa muda mrefu

Pamoja na sababu hizo, pia tatizo hilo huweza kuwa dalili za ujauzito kwa kinamama au kunashida nyingine zaidi ambayo huhitaji uchunguzi wa kitaalam zaidi.

Lakini unaweza kutumia kitunguu swaumu kama huduma ya kwanza pale unapopatwa na maumivu makali ya kiuno. Unachopaswa kufanya ni kutafuta kitunguu swaumu kisha pondaponda punje moja ya kitunguu swaumu na kupaka sehemu ya kiuno inayouma kabla ya kwenda kulala.

Maumivu yanapozidi unaweza kufika kwenye kituo cha afya kilicho karibu nawe au tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment