Saturday, 8 July 2017

Juisi zipo nyingi, lakini leo zifahamu faida za hii juisi ya boga

MABOGA hutokana na tunda liitwalo boga. Tunda hilo asili yake haijafahamika vizuri ingawaje baadhi ya tafiti zinasema asili yake ni Amerika Kaskazini.

Zao la maboga mara nyingi hushamiri zaidi katika msimu wa joto na inashauriwa kupanda zao hili mwanzoni mwa mwezi Julai hasa katika udongo unaotunza maji vizuri.

Maboga ni moja ya chakula bora na muhimu kwa siha ya mwili wa mwanadamu endapo yataandaliwa vizuri.

JUISI YA BOGA

Juisi ya boga ina uwezo mkubwa wa kupambana na shinikizo la juu damu pale unapokunywa mara kwa mara hii ni kwa sababu ndani ya boga kuna kirutubisho kiichacho 'pectin' ambacho hufanya kazi ya kushusha 'cholesterol' na hivyo kupambana na matatizo ya shinikizo la damu.

Aidha, matumizi ya juisi hii ni muhimu pia kwa afya ya figo na ini ikiwa mhusika atatumia kwa uaminifu mara tatu kwa siku yaani asubuhi mchana na jioni kila siku.

Mbali na hayo, juisi hiyo hurekebisha mmeng'enyo wa chakula tumboni, 'digestion system' kutokana na kuwa na kiwango cha nyuzinyuzi 'fiber'.

Kumbuka kwamba, mbegu za maboga huweza kufanya vizuri endapo zikitumika zikiwa hazijaoza na zisizo kaa kwa muda mrefu.

Mtuamiaji anapaswa kutumia mbegu hizo kwa usalama zaidi baada ya kuziosha kwa maji safi na salama kisha zianikwe na inapendeza zaidi mtumiaji akala bila kukaanga.

Pia baada ya kukaanga unaweza kupata faida. Inashauriwa kuwa upokaanga mbegu za maboga usitumie zaidi ya dakika 10.

Kwa maelezo zaidi au ushauri unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment