Saturday, 8 July 2017

Kama huwa unasumbuliwa na maumivu ya hedhi soma hapa


Mara nyingi wnawake wengi wakati wa hedhi, huhisi maumivu kidogo au makali na kusababisha kukosa raha na kushindwa kabisa hata kufanya shughuli nyingine muhimu.

Baadhi ya wanawake wanapokaribia kuingia katika siku zao misuli hubana na maumivu ya mapaja na miguu.

Lakini wakati mwingine hali huwa inakuwa mbaya zaidi ambapo mhusika anapata maumivu makali ya mgongo, tumbo na hata maumivu wakati wa kutoa damu.

Sasa basi Mtaalam Mandai kutoka Mandai Products Ltd anasema kwamba tangawizi inaweza kuwa suluhisho la tatizo la maumivu hayo makali wakati wa hedhi kwako mwanamke.

Unachotakiwa kufanya ni kupondaponda (saga) tangawizi mbichi, kisha chemsha maji ya kutosha kwa dakika kumi. Ongeza sukari kidogo halafu chuja.

Tumia glasi moja ya maji hayo mara tatu kwa siku hususani mara baada ya kula.

Njia hii ni vyema ikaanza siku tatu kabla ya hedhi na kipindi chote cha hedhi ili kupunguza makali ya maumivu hayo.

Unaweza pia kupokea ushauri wa bure kutoka kwetu kuhusu masuala ya lishe bora tupigie sasa kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com tupo kwaajili yako karibu.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment