Thursday, 27 July 2017

Kazi 3 muhimu za boga kwenye afya yako

Boga ni mojawapo ya tunda zuri na lenye virutubisho vingi ambavyo vyote ni muhimu sana kwa afya ya miili yetu.

Kama utakuwa ni mfuatiliaji wa masomo yetu a kwa mara kupitia tovuti hii nadhani utakuwa unakumbuka kuwa mara kadhaa tumeshazungumza kuhusu faida za boga kwa ujumla, lakini hiyo haizuii kuendelea kuzungumzia sifa za boga leo tena.

Leo napenda tuzungumzie uwezo wa boga katika kuboresha afya ya ngozi zetu kama ifuatavyo>>
Kwanza kabisa unapotumia boga husaidia kuleta unyevunyevu kwenye ngozi na hivyo kuwasaidia wale wenye ngozi kavu hii ni kutokana na kuwa na vitamin E ya kutosha pamoja na kirutubisho kiitwacho 'antioxidant '

Maboga pia yana vitamin A yakutosha ambayo husaidia kulinda ngozi dhidi ya kuharibika na kuunda seli mpya ndani ya ngozi.

Lakini pia ndani ya boga kuna vitamin C ambayo nayo huhitajika katika kuhakikisha afya ya ngozi inakaa vizuri zaidi siku zote

Unayo nafasi ya kutuuliza chochote kuhusu masuala ya lishe na afya yako kwa ujumla tupigie kwa namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment