Monday, 24 July 2017

Kitunguu swaumu kinavyoweza kumaliza majeraha


KITUNGUU swaumu ni miongoni mwa viungo vinavyotegemewa katika kuongenza ladha nzuri kwenye vyakula mbalimbali.

Mbali na kiungo hicho kutumika kunogesha vyakula pia kikitumiwa ipasavyo huweza kusaidia kutoa ahueni kwa matatizo mbalimbali ya kiafya.

Kiungo hiki husaidia kupunguza shida ya kubanwa na pumu au kushindwa kupumua, lakini pia kitunguu swaumu husaidia kutibu majeraha yatokanayo na kuumwa na wadudu kama ng'e ambapo ili utumie kiungo hiki kama tiba utapaswa kukisaga kisha utabandika sehemu yenye tatizo.

Kitunguu swaumu pia husaidia kutoa ahueni kwa wenye matatizo ya ngozi hususani yenye vilenge lenge ambapo dalili zake ni madoa meupe yenye magamba (huchunika kama ngozi iliyoungua) mikononi, miguuni, shingoni au usoni. Hivyo matatizo yote hayo huweza kupatiwa suluhisho kwa kutumia kitunguu swaumu.

Matumizi ya kitunguu swaumu ni msaada pia kwa watu wenye matatizo ya kukosa choo kwa muda wa siku mbili au zaidi.

Maumivu ya kiuno nayo huweza kupatiwa ufumbuzi kwa kutumia kiungo hiki, lakini pia kitunguu swaumu kinaweza kutumika kama njia ya kusafisha vidonda kutokata na uwezo wake wa kuua vijidudu au bakteria. Ili kutumia kiungo hiki katika hili mhusika atapaswa kusaga kitunguu swaumu na kukibandika sehemu ya kidonda kwa muda usiopungua dakika kumi na baadaye kutoa. Ni kizuri hata kwa vidonda ndugu.

Katika tafiti mbalimbali vitunguu swaumu vinaelezwa kuwa na uwezo wa kutoa ahueni kwa wenye maambukizi ya bakteria, fangasi pamoja na virusi tofauti tofauti.

Mbali na hayo, kitunguu swaumu huweza kutumika kama njia ya kuboresha afya ya mwili na hivyo kumfanya mtumiaji kuwa mrembo. Kwenye haya masuala ya urembo kiungo hiki huweza kuwa msaada kwa wale wenye matatizo ya chunusi. Ili kumaliza shida hiyo ya chunusi mhusika atachanganya kitunguu swaumu kilichosagwa pamoja na kijiko cha juisi ya ndimu. Kisha chukua pamba na upake sehemu iliyoathirika.

Hata hivyo, si vizuri kutumia kiungo hiki bila kupata ushauri wa wataalamu wa tiba zitokanazo na mimea au tiba asili wanaotambulika kisheria.

Madhara yanayoweza kuchangiwa na kitunguu swaumu

Kitunguu swaumu kama kikitumika bila maelekezo ya wataalam huweza kusababisha madhara yafuatayo:

Huweza kuchangia mhusika kuhisi kichefuchefu na wakati mwingine kutapika na kuharisha.

Pia huweza kusababisha hatari ya mhusika kuvuja damu kutokana na kuzuia seli sahani ambazo husaidia damu kuganda kushindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi wake wa kawaida.

Hivyo, kiungo hiki hakishauriwi kutumiwa kwa akinamama wajawazito au waliotoka kujifungua.

Kutokana na hayo ni vema ukaepuka kutumia kitunguu swaumu bila kupata ushauri kutoka kwa wataalam kwani huweza kuwa na madhara kwa afya yako.

Kwa ushauri zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment