Friday, 14 July 2017

Maajabu 6 yatokanayo na kula kabeji nyekundu


Kabeji ni miongoni mwa mboga mabayo wengi tunaifahamu lakini si wote tunafahamu manufaa yake ndani ya miili yetu.

Leo nataka kuzungumzia kuhusu kabeji nyekundu ambayo inasifika kwa kuna na utajiri wa madini na vitamin mbalimbali ambazo ni muhimu kwa miili yetu.

Miongoni mwa faida za kabeji nyekundu ni pamoja na hizi zifuatazo:

1. Kuboresha afya ya macho.
Ulaji wa kabeji hii hufaa kwa afya ya macho kutokana na kabeji hii kuwa na  kirutubisho cha 'zeaxanthin' na  'lutein' ambazo huenda kusaidia kuyalinda macho dhidi ya miale iitwayo 'Ultraviolet radiation'  (UV.)

2. Huboresha afya ya moyo
Sababu nyingine ya kula kabeji nyekundu ni kwasababu juisi yake husaidia uundajiwa seli nyekundu za damu mwilini, pamoja na kupunguza kiwango cha sumu mbalimbali mwilini hali ambayo husaidia mzunguko wa damu mwilini kuwa vizuri.

3. Huimarisha kinga za mwili
Hii ni kutokana na kuwa na vitamin C ya kutosha, hivyo unapotumia kabeji nyekundu husaidia mwili kujiwekea uhakika wa kujikinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.

4. Hufanya ngozi kuendelea kuonekana vizuri
Kabeji ya kijana huimarisha afya ya ngozi kwakuwa ndani yake ina vitamin C, E na A ambazo hujenga vyema afya ya ngzoi

5. Ni msaada kwa wenye kisukari
Kabeji nyekundu huweza kuwasaidia wenye kisukari kutokana na kuwa na insulin yake ya asili.

6. Huboresha afya na mifupa
Kabeji hii inawingi wa vitamin K ambayo husaidia kujenga na kuimarisha afya ya mifupa.

Unaweza pia kupokea ushauri wa bure kutoka kwetu kuhusu masuala ya lishe bora tupigie sasa kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com tupo kwaajili yako karibu.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku


No comments:

Post a Comment