Wednesday, 5 July 2017

Maji ya njegere huweza kuwasaidia wenye tetekuwanga


Tetekuwanga huu ni ugonjwa ambao hautofautiani sana na surua kutokana na ugonjwa huu nao kuwashambulia sana watoto wenye umri wa chini ya miaka saba.

Ugonjwa huu unaambukiza kwa haraka sana, hususani pale ambapo unaonekana kwamba unaelekea kupona.

Dalili za tetekuwanga ni pamoja na hali ya kuhisi kuwa na homa, kuumwa kichwa, kusikia uchovu wa mwili, kuonekana kwa vipele kifuani aua sehemu ya juu ya mgongo na hatimaye upele unaofanana na malengelenge husambaa mwili mzima.

Hata hivyo, baada ya siku chache upele huo hutumbuka na kuanza kukauka na hapo mgonjwa huweza kuanza kupona kwa kipindi cha siku kumi hadi ishirini.

Moja ya mbinu ambayo huweza kupunguza madhara ya tetekuwanga ni pamoja na matumizi ya njegere.

Unachotakiwa kufanya ni kupata njegere zako kisha chemsha kama kawaida baada ya njegere zako kuiva utachuja yale maji na kunawia sehemu zilizoathirika kwa tatizo. Hii ni kwasababu maji hayo ya njegere huwa na vitamin mbalimbali na madini ambayo huwa na nafasi ya kuuongezea mwili uwezo wa kupambana na maambukizi.

Kwa ufafanuzi zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandatz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment