Tuesday, 18 July 2017

Mambo 3 yanayochangia mwanamke anayenyonyesha kukauka maziwa

Mara kadhaa tumekuwa tukipokea malalamiko ya kutotoka kwa maziwa kwa kinamama wanaonyonyesha, hali ambayo pia huchangia hata afya ya mtoto kudhorota.

Kuna baadhi ya wanawake hujikuta wakiingia kwenye tatizo hili la maziwa kushindwa kutoka au kutoka kwa uchache sana kutokana na kubanwa na kazi zao za kila siku na hivyo kufanya mwili maziwa kutoka kwa uchache zaidi au kutotoka kabisa.

Sasa hapa zipo sababu ambazo huchangia tatizo hilo kwa kinamama:-

Kutokula vizuri
Uwingi wa maziwa ya mama au uchache hutegemea sana na namna mama anavyokula, endapo mama hana jitihada za kula basi pia huweza kuchangia uchache wa maziwa kwa mama husika, lakini kama mama anakula kiasi cha kutosha basi kuna uwezekano mkubwa wa maziwa kuwa yakutosha pia.

Kutonyonyesha kiasi cha kutosha
Kimsingi mama anapaswa kunyonyesha angalau mara mara 10 na kuendelea kwa siku. Kitendo cha kunyonyesha mara kwa mara mwili hujenga utaratibu wa kutengeneza maziwa kila unapohisi hakuna maziwa kwenye matiti, lakini mwili unapohisi kwenye matiti tayari kuna maziwa huwa kunaonekana hakuna haja ya kutengeneza tena maziwa. Hivyo ni muhimu kunyonyesha mara kwa mara kila siku.

Matumizi ya dawa
Kuna baadhi ya dawa zinapotumiwa na mama anayenyonyesha huweza kuathiri mfumo mzima wa utengenezaji maziwa ndani ya mwili na hivyo kuchangia mama kukosa maziwa ya kumyonyesha mtoto, inapotokea hali kama hii ni vyema kuonana na wataalam wa afya kwa ushauri zaidi.

Kwa ushauri zaidi tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment