Friday, 14 July 2017

Mambo 5 hatari ambayo huchangiwa na kuvaa nguo za kubana


Kuna baadhi ya mavazi huweza kumuingiza mvaaji kwenye matatizo ya afya kadhaa endapo mavazi hayo yatavaliwa mara kwa mara.

Miongoni mwa mavazi hayo ni pamoja na zile nguo ambazo hubana sana ambazo mara nyingi huvaliwa na kinadada na mara chache kwa baadhi ya vijana wa sasa wa kizazi kipya.

Miongoni mwa madhara yanayoweza kusababishwa na kuvaa mavazi ya kubana ni pamoja na haya yafuatayo:-

1. Rahisi kusababisha maambukizi
Mavazi yanayobana sana hasa kwa wanawake huweza kurahisisha urahisi wa mhusika wa kukumbwa na maambukizi kirahisi hasa yale ya sehemu za siri.

2. Mzunguko hafifu wa damu mwilini
Pale mtu anapovaa nguo inayombana sana huweza kuchangia mwili kutokuwa na mzunguko mzuri wa damu mwilini kwasababu mishipa ya damu inakuwa imebanwa sana. Kutokana na hali hiyo mhusika pia huweza kupatwa na tatizo la kuhisi uchovu mara kwa mara.

3.Umeng'enyaji wa chakula kuwa hafifu.

Unapokuwa umevaa nguo ya kubana huweza kuchangia mwili kutokuwa sawa mara baada ya kutoka kula kwasababu tumbo linaweza kubanwa sana na hivyo kutorahisisha mfumo mzima wa umeng'enyaji wa chakula na hivyo hata kupelekea tatizo la kukosa choo.

4. Ugumu wa kupumua
Tambua kuwa unapovaa nguo za kubana unaweza kubana sehemu yako ya kifua au mapafu na hivyo kuchangia kuathiri kwa namna moja au nyingine mfumo mzima wa upumuaji.

5. Maumivu ya misuli

Uvaaji wa nguo za kubana pia huchangia misuli kuuma na hivyo kuchangia hata mwendo wako kubadilika kwa wakati fulani fulani.

Kwa maelezo zaidi au ushauri unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment