Wednesday, 5 July 2017

Mambo 6 ya kufanya ili kuongeza kinga zako za mwili


Kinga za mwili ndio msingi afya ya binadam kwani unapokuwa na kinga imara pia husaidia kuimarisha afya ya mwili kwa ujumla na kutozongwa na magonjwa hovyo..

Leo nataka kukwambia mambo ya kufanya endapo utagundua kuwa kinga zako za mwili zimeshuka.

1. Punguza mawazo 'stress' 
Msongo wa mawazo wa mara kwa mara ni miongoni mwasababu ambazo huweza kuchangia kuendelea kushuka kwa msongo wa mawazo. Hivyo ni vyema kuepuka msongo huo wa mawazo.

2. Lala kiasi cha kutosha
Ili kuepuka kuendelea kushuka kwa kinga za mwili jitahidi kupata muda wa kupumzisha mwili kiasi cha kutosha ikiwa ni pamoja na kulala

3. Zingatia mlo kamili
Unahitaji kuzingatia aina ya vyakula unavyokula ili kuimarisha kinga za mwili zaidi epuka ulaji wa vyakula vya viwandani

4. Epuka vitu vya anasa
Ikiwa kinga zako za mwili zimeshuka jitahidi kuepuka matumizi ya pombe au sigara ambayo huweza kuchangia madhara zaidi ikiwa ni pamoja na kuendelea kushuka kwa kinga za mwili

5. Zingatia unywaji wa vyakula vyenye asili ya maji maji

6. Fanya mazoezi
Mazoezi pia huweza kukusaidia kuimarisha zaidi kinga zako za mwili

Kwa ufafanuzi zaidi na maelezo zaidi unaweza kuwasiliana nasi kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment