Saturday, 15 July 2017

Maswali 5 yakujiuliza kabla ya kuanzisha mahusiano mapya

Picha kwa msaada wa mtandao
Kuanzisha mahusiano ni moja ya changamoto kwa watu wengi kwani endapo mhusika anapokuwa hayupo makini huweza kujikuta akiingia kwenye mahusiano ambayo hakuyatarajia hapo awali.

Hivyo kuna mambo mengi ya kuzingatia kabla ya kuamua kuanzisha mahusiano mapya, miongoni mwa maswali ambayo unatakiwa kujiuliza kabla ya kuanzisha mahusiano mapya ni pamoja na haya yafuatayo;-

1. Je, upo tayari kuanzisha mahusiano mapya kwa wakati huo.
Swali hili linamaana kubwa hupaswi kukulupuka bali unapaswa kutathimini maamuzi yako vyema kabla ya kuamua kuingia kwenye mahusiano mapya na mtu mwingine.

2. Jiulize kama tayari umeachana kabisa na mpenzi wako wa zamani
Kuna wale ambao wanafanya maamuzi ya kuachana wakiwa na hasira halafu baadaye wanaanza kujuta na kutamani kurudi kwa wenzi wao wa zamani, hii huweza kukusababishai madhara hasa msongo wa mawazo, hivyo kabla ya kuanza mahusiano mapya jihakikishie kabisa uliyekuwa naye awali umeachana naye kabisa.

3. Fikiria kipi ulifanya na kipi hukufanya kwenye mahusiano yako yaliyopita
Hii itakusaidia kuwa na mahusiano mazuri zaidi kwenye mahusiano mapya kwani utakuwa unajua nini kizuri na kibaya cha kufanya kwenye mahusiano yako mapya.

4. Jiulize unahitaji mahusiano ya aina gani
Kwa kifupi swali hili linamaana kuwa ni kwa kiasi gani unadhani ni muhimu kuwa na mahusiano mapya na si kukaa pekee yako

5. Unahitaji nini nje ya mahusiano hayo mapya.
Inawezekana unataka kuanzisha mahusiano mapya kwa kuwa kuna baadhi ya vitu unavikosa kwenye mahusiano ya sasa mfano unakosa uaminifu, ukweli, ucheshi n.k.

Unaweza kupata ushauri zaidi kutoka kwetu kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment