Saturday, 1 July 2017

Mbinu 3 za kuwasaidia wenye tatizo la kuona mbali


Ikiwa huwa unapata shida ya kuona mbali katika maisha yako au shughuli mbalimbali za kikazi na kimasomo basi si jambo la kulichukulia mzaha.

Unapoona hali hiyo jitahidi uwaone wataalam wa afya ya macho kwa ushauri zaidi, lakini pia unaweza kutumia njia hizi nyingine asili ili kupata ahueni zaidi.

1. Ulaji wa matunda na mbogamboga
Unatakiwa kuzingatia ulaji wa mbogamboga na matunda ili kuboresha afya ya macho hii ni kwasababu matunda na mbogamboga huwa na vitamin A,B, C, D na E ambazo ni vitamin muhimu kwa afya ya macho.

2. Tui la nazi
Hii ni njia nyingine asili ya kuboresha afya ya macho hii ni kwasababu kimiminika hicho kina vitamin B1, B3, B5, B6 pamoja na madini ya chuma, calcium, sodium na selenium, magnesium n.k Miongoni mwa vitamin na madini tajwa hapo juu ni mazuri kwa afya bora.

3. Karoti
Karoti inawingi wa beta carotene ambayo husaidia uundaji wa vitamin A ambayo ni vitamin muhimu kwa afya ya macho.

Unaweza kuwasiliana nasi kwa ushauri zaidi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandatz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment