Monday, 31 July 2017

Mwanamke: Aina 3 ya vyakula vyenye kuondoa harufu mbaya sehemu ya siri

Kama utakuwa ni mfuatiliaji mzuri wa tovuti hii bila shaka utakumbuka kuwa tayari tumeshaelezana kuhusu sababu ambazo hupelekea mwanamke kutokwa na majimaji yenye harufu sehemu za siri.

Sasa ni hatua ya kufahamu njia ambazo huweza kusaidia kukabiliana na tatizo hilo, karibu tuzifahamu hapa chini kwenye orodha hii hapa.

1. Kutumia uwatu (fenugreek seeds) 
Tafuta mbegu kadhaa za uwatu weka kwenye glasi yenye maji kisha acha zilale humo halafu kesho yake asubuhi kunywa maji hayo kabla ya kula chochote. Fanya zoezi hilo ndani ya siku kadhaa.

2. Tumia mchanganyiko wa maziwa & binzari
Changanya kijiko kimoja cha chai cha binzari au manjano kwa jina jingine kisha chukua kikombe kimoja cha maziwa ya moto na unywe yote. Fanya zoezi hilo hadi pale tatizo litakapoisha.

3. Juisi ya Komamanga.
Juisi hii inavirutubisho vingi ambavyo huweza kusaidia kutoa ahueni kwa mwanamke mwenye shida ya kutokwa na maji machafu sehemu za siri. Kunywa juisi hiyo mara kwa mara ili kupata mafanikio zaidi.

Endelea kufuatilia mtandao huu baadaye tutafahamishana mambo ya kufanya ili kuepuka tatizo hili la kutokwa na maji yenye harufu sehemu za siri kwa wanawake. Pia unaweza kutupigia kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pep dkmandaitz@gmail.com

Pamoja na hayo, bado unaweza kupakua Application yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment