Saturday, 1 July 2017

Njia 4 za kupunguza lehemu (sumu) mwilini


Lehemu mwilini au 'cholesterol' ni moja ya tatizo ambalo wanaweza kuwa nalo watu wengi, wingi wa cholesterol mwili huweza kusababisha madhara kwa afya ikiwa ni pamoja na magonjwa ya moyo.

Sababu kubwa za lehemu kuongezeka mwilini ni pamoja na moshi, unene kupita kiasi, kisukari, matatizo ya figo, ini nk.

Kwa kawaida ni vyema kuhakikisha mwili wako hauna kiwango kikubwa cha lehemu na hapa ninazo njia ambazo huweza kusaidia kupunguza kiwango cha lehemu mwilini.

1. Kitunguu maji
Onion
Juisi ya kitunguu maji huweza kutumika kama moja ya njia ya kupunguza kiwango cha lehemu mwilini endapo itaandaliwa vizuri.

2. Juisi ya chungwa
Orange Juice
Juisi hii ina vitamin C, pamoja na madini ya 'folates' na 'flavonoids'  uwepo wa vitamini hiyo na madini hayo husaidia kupunguza kiwango cha lehemu mwilini.

3. Mafuta ya nazi
Coconut Oil
Mafuta haya nayo huweza kutoa ahueni kwa wenye shida ya tatizo la lehemu mwilini, hivyo mafuta hayo huweza kutumika kuandalia baadhi ya vyakula.

4. Mafuta ya samaki

Mafuta haya yanautajiri wa kirutubisho cha omega 3 ambacho ni kirutubisho kizuri cha kupunguza lehemu mwilini.

Unaweza kuwasiliana nasi kwa ushauri zaidi kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandatz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment