Monday, 31 July 2017

Orodha ya vyakula & matunda ambavyo hutuliza maumivu ya tumboMmeng'enyo wa chakula tumboni ni moja ya suala muhimu sana kwa afya zetu wanadamu kwani chakula kinapomeng'enywa vizuri huufanya mwili kupata virutubisho vyote muhimu ndani ya mwili.

Pia  umeng'enyaji mzuri wa chakula husaidia kupunguza maudhi mbalimbali mwilini ikiwa ni pamoja na maumivu ya tumbo na mara nyingine tumbo kujaa gesi.

Leo naomba tuelezane baadhi ya vyakula ambavyo husaidia kuimarisha au kuboresha mfumo mzima wa mmeng'enyo wa chakula.

1. Tangawizi

Unachoweza kufanya ni kusaga tangawizi kisha tengeneza chai yake na utumia kikombe kimoja kila siku ambacho kitakusaidia kuboresha afya ya mmeng'enyo wa chakula.

2. Kiazi kitamu

Kiazi hiki hufaa zaidi kuimarisha mmeng'enyo wa chakula kutokana na kuwa na 'starch' ambayo husifika kwa kuboresha mfumo huo muhimu wa mwili.

3. Parachichi

Tunda hili licha ya ladha yake nzuri, lakini pia linasifika kwa kuwa na nyuzinyuzi ambazo husaidia kurahisisha mfumo mzima wa mmeng'enyo wa chakula.

4.Apple/ tufaa
apples
Tunada hili ni nzuri kwa mfumo wa ummeng'enyaji wa chakula kutokana na kuwa na nyuzinyuzi pia ndnai yake.

5. Ndizi
bananas
Tuna hili nalo hufaa katika kuboresha mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na ni tunda nzuri pia kwa wale wenye shida ya kuhara kutokana na kuwa na madini yakutosha ya potassium ambayo hupotea zaidi pale mtu anapoharisha.

Kwa ushauri zaidi tupigie kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com au fika ofisi zetu Makao makuu Ukonga, Mombasa mtaa wa Mongolandege jijini Dar es Salaam.

Pamoja na hayo, bado unaweza kupakua Application yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment