Saturday, 29 July 2017

Samaki anavirutubisho vyake muhimu pia


MATUMAINI yangu kuwa u mzima mpendwa msomaji wetu wa www.dkmandai.com. Leo pamoja napenda tufahamishane jinsi kitoweo cha samaki kinavyoweza kuimarisha afya yako.

Vyakula vya baharini ni miongoni mwa vyakula muhimu sana katika kuimarisha afya ya ngozi.

Vyakula hivi hufaa kwa afya ya ngozi kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha Zinc na Omega 3 ambazo ni muhimu kwa siha ya ngozi.

Faida za Omega 3 ni pamoja na kuondoa kukakamaa au ukavu wa ngozi na kupunguza kuvimba na kukunjamana kwa ngozi.

Pia husaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini hivyo kuboresha ngozi. Damu inapozunguka vyema mwilini afya ya ngozi nayo huimarika. Zinc nayo husaidia kuondoa harara na chunusi katika ngozi kwasababu huyeyusha homoni ya testosterone. Pia husaidia kuzalishwa seli au chembe hai za mwili na kuondoa chembe zilizokufa huku ikiifanya ngozi ing'ae na kuwa na mvuto zaidi.

Kwa maelezo zaidi wasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

No comments:

Post a Comment