Tuesday, 18 July 2017

Unajua faida hizi 4 za mbegu za ukwaju

Ukwaju ni tunda linalotokana na mkwaju, mkwaju ni mti unaotoa matunda ambayo yanajulikana kama ukwaju ambayo wengi huyatumia kwa kula au kutengenezea juisi.


Bila shaka kumekuwepo na watu wengi ambao hutumia tunda hili lenye ladha ya ugwadu (uchachu) kwa kutengenezea hasa juisi ambayo hutumika kama kinywaji kinachoburudisha.


Hata hivyo, leo sina lengo la kuzungumzia kuhusu ukwaju, bali napenda kukwambia kuhusu faida za mbegu za ukwaju.


Mbegu za ukwaju zinavirutubisho mbalimbali ikiwa ni pamoja na madini ya calcium, potassium, magnesium, phosphorus na vitamin C.


Miongoni mwa faida za mbegu hizi za ukwaju ni pamoja na hizi zifuatazo:


1. Kupunguza maumivu ya viungo, unachopaswa kufanya ni kusaga mbegu hizo kisha tumia kwa kuchanganya na maji halafu kunywa kutwa mara mbili kwa siku.


2. Huboresha umeng'enyaji wa chakula tumboni, tumia unga wa mbegu zake uliosagwa na kisha kuchanganywa na maji kunywa maji hayo angalau kila siku ili kuboresha umeng'enyaji wa chakula tumboni.


3. Huongeza uwezo wa kinga za mwili na hivyo kumfanya mhusika kuwa naq kinga imara za kupambana dhidi ya magonjwa.


4. Pamoja na hayo mbegu hizi pia husaidia wenye tatizo la kikohozi, tonsil pamoja na kuboresha afya ya ngozi kwa ujumla.


Unaweza kupata ushauri zaidi kutoka kwetu kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore ya simu yako kisha tafuta Mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment