Friday, 14 July 2017

Vifahamu viungo 2 vyenye sifa ya kuondoa maumivu ya mwili haraka


Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakisumbuliwa na maumivu sugu ya sehemu mbalimbali za miili yao, mauimivu hayo huweza kuwa ya miguu, mgongo, kiuno n.k .

Inawezekana maumivu hayo yamekusumbua kwa mda mrefu na umeshatumia dawa nyingi bado hujapata nafuu na sasa umeamua kuliita tatizo lako ni sugu.

Sasa leo msomaji wangu naomba ni kwambie hivi viungo viwili ambavyo vitaweza kukusaidia kumaliza au kupunguza hayo maumivu yako unayoyaita sugu.

1. Manjano/ binzari

Kiungo hiki licha ya kutumika zaidi kwenye matumizi ya jikoni, lakini pia hufaa kutuliza maumivu ya sehemu mbalimbali za mwili yakiwemo yale sugu . Unachotakiwa kufanya ni kuchanganya unga wa binzari pamoja na asali kiasi kidogo kisha tumia mchanganyiko huo kupaka sehemu iliyoathirika au yenye maumivu.

2. Tangawizi

Hiki nako ni kiungo kizuri ambacho huongeza ladha kwenye vimiminika ikiwa ni pamoja chai, lakini pia kiungo hiki huweza kusaidia kutuliza maumivu ya viungo ikiwa utakiandaa vizuri.

Unachotakiwa kufanya pia ni kupata unga wa tangawizi halisi kisha weka na asali kiasi kidogo halafu utatumia mchanganyiko huo kuchua taratibu sehemu yenye tatizo.

Kwa maelezo zaidi au ushauri unaweza kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200, 0784 300 300, 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku

No comments:

Post a Comment