Saturday, 15 July 2017

Vyakula & vinywaji vyenye uwezo wa kutuliza maumivu ya tumbo


Inawezekana kuna wakati huwa unapatwa na maumivu ya tumbo na unashindwa kujua nini ule au unywe ili kupunguza maumivu hayo.

Maumivu ya tumbo huweza kusababishwa na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kula chakula chenye sumu, kichafu, kilichoharibika n.k

Leo ninayo hii orodha ya vyakula vyenye uwezo wa kukusaidia kutuliza maumivu ya tumbo.

1. Ndizi

Tunda hili huweza kupunguza maumivu ya tumbo kwa kuwa lina nyuzinyuzi ambazo kwa namna moja au nyingine huweza kuchangia kutuliza maumivu ya tumbo.

2. Rojo la tufaa (apple)

Ukipata tunda la tufaa lililosagwa na ukala husaidia kukata maumivu ya tumbo haraka zaidi.

3. Supu ya mbogamboga

Hii ni supu nzuri hasa kwa wale wenye shida ya mmeng'enyo mbovu wa chakula, lakini pia husaidia kutuliza maumivu ya tumbo kwa haraka.

4. Maji ya nazi

Maji haya nayo huweza kutumika kutuliza maumivu ya tumbo na kuimarisha mfumo wa umeng'enyaji wa chakula tumboni. Maji haya huwa na vitamin C, pamoja na madini ya potassium.

5. Tangawizi

Kiungo hiki huweza kupunguza maumivu ya tumbo kwa haraka pamoja na kuimarisha kinga za mwili.

Unaweza pia kupokea ushauri wa bure kutoka kwetu kuhusu masuala ya lishe bora tupigie sasa kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com tupo kwaajili yako karibu.

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa zetu kupitia simu yako kila siku.

No comments:

Post a Comment