Monday, 24 July 2017

Vyakula vya kutumia kwa wanawake wenye uzazi wa mbali!

Kupata mtoto ni moja ya jambo muhimu na la furaha katika familia yoyote, licha ya kwamba kwa baadhi ya wanafamilia jambo hili limekuwa changamoto kwao.

Leo ninayo orodha ya vyakula ambavyo huweza kusaidia kuweka uzazi kuwa wa karibu zaidi.

1. Mayai
Mayai yamesheheni virutubisho vya aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na vitamin D ambayo husaidia kuhamasisha uzazi kuwa karibu. Kwa mujibu wa utafiti uliowahikufanywa katika chuo cha Yale University ambapo walibaini kuwa wanawake wenye upungufu wa vitamin D huweza kupatwa na changamoto ya uzazi.

2. Samaki
Samaki nao husogeza karibu uzazi kwa wale wenye uzazi wa mbali kutokana na kitoweo hicho kuwa na kirutubisho cha omega 3 ambayo husaidia kurekebisha homoni za masuala ya uzazi ndani ya mwili, lakini pia huongeza mzunguko wa damu kwenda kwenye viungo vya uzazi.

3. Parachichi
Hili ni tunda muhimu pia kwa masuala ya uzazi kutokana na kuwa na virutubisho vya folic acid, monounsaturated fat pamoja na vitamin B ambazo kwa pamoja husaidia kuamsha homoni za uzazi kwa wanawake na wanaume.

Monounsaturated fat ambayo hupatika kwenye parachichi husaidia kurekebisha homoni ambazo husimamia masuala ya uzazi ndani ya mwili na hivyo kuongeza uwezekano wa kushika ujauzito kirahisi zaidi.

4. Broccol
Hii ni aina ya mbogamboga ambayo ndani yake imesheheni kiwango kikubwa cha vitamin C ambapo vitamini hiyo ni miongoni mwa vitu muhimu kwenye suala ya uzazi kwani husaida mwanaume kuwa na manii yenye uwezo wa kutungisha mimba , lakini kwa wanawake huweza kusaidia kutoharibika kwa mimba mara kwa mara.

Lakini pia kama unasumbuliwa na tatizo hili unaweza kusoma hapa chini

Kwa maelezo zaidi usisite kuwasiliana na Mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0769 400 800/ 0784 300 300 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com.

No comments:

Post a Comment