Advertisement

Advertisement

.

.

Mixer

Mixer

Wednesday, 30 August 2017

Aina 2 ya vinywaji vyenye uwezo wa kulinda afya ya figo

pomegranate juice 620
AFYA ya figo ni muhimu kama ilivyo afya ya moyo, hii ni kwa sababu figo ni moja ya kiungo ambacho husaidia kuchuja sumu mbalimbali ndani ya mwili na baadaye kutoa taka mwili kwa njia ya haja ndogo (mkojo)


Matatizo ya figo huweza kuchangia ugumu wa upatikanaji wa haja ndogo (mkojo) au miguu na mikono kuvimba.

Pia mtu mwenye shida ya figo huwa katika hatari kubwa ya kukumbwa na matatizo ya moyo.

Leo nimeona nikwambie kuhusu hivi vinywaji viwili ambavyo huweza kumsaidia mtu mwenye shida ya mawe kwenye figo.

1. TikitimajiMatumizi ya tikiti maji huweza kuwa msaada kwa mtu mwenye shida ya mawe kwenye figo kutokana na kuwa na madini ya potassium, chumvi ndani yake ambayo husaidia kurekebisha kiwango cha acid kwenye haja ndogo (mkojo). Hata hivyo matokeo mazuri ya juisi hii utaweza kuyapata endapo itachanganywa na kiungo fulani ambacho sana sana hutumiwa na wahindi.

2. Juisi ya Komamanga
 Mbegu pamoja na juisi ya komamanga ni vitu muhimu sana kwa afya ya figo kutokana na uwezo wake wa kuondoa mawe kwenye figo. Hii ni kutokana na juisi hiyo kuwa ni chanzo kizuri cha madini ya potassium.

Asante kwa kuendelea kufuatilia mtandao huu kwa mengine zaidi unaweza kuwasiliana na mtaalam Mandai kwa simu namba 0716 300 200/ 0784 300 300/ 0769 400 800 au barua pepe dkmandaitz@gmail.com

Pia unaweza kupakua App yetu kwa kuingia kwenye playstore kisha tafuta mandai products na utaidownload kisha utakuwa unapata kila taarifa kwenye simu yako kutoka kwetu kila au kila mara tutakapokuwa tunapost.

No comments:

Post a Comment